• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kufanya maombi ya kitaifa kuhusu janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-12 08:53:48

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ameitangaza Juni 15 kuwa siku ya kitaifa ya maombi na kufunga dhidi ya janga la COVID-19.

    Zimbabwe imeshuhudia kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika wiki za karibuni, kufuatia raia wengi kurudi kutoka nchi jirani.

    Rais Mnangagwa amesema raia wanapaswa kushiriki kwenye maombi ya kitaifa kwa familia na kwa vikundi vidogo vya watu wasiozidi 50, na pia wanatakiwa kuchukua tahadhari ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako