• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya, Tanzania na Uganda zatangaza bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/21

    (GMT+08:00) 2020-06-12 09:08:19

    Tarehe 11 Juni, nchi tatu za Afrika Mashariki, Kenya, Tanzania na Uganda zimetangaza bajeti zao za mwaka wa fedha wa 2020/21.

    Kenya imetangaza bajeti ya shilingi trilioni 2.7 ambayo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, ili kukuza uchumi baada ya nchi hiyo kuathiriwa na COVID-19, uvamizi wa nzige na mafuriko. Waziri wa fedha wa nchi hiyo Bw. Ukur Yatani amesema, athari hizo zitasababisha makadirio ya awali ya ongezeko la uchumi ambayo ni asilimia 6.1 kushushwa hadi asilimia 2.5, lakini yanatarajiwa kuongezeka mwaka 2021.

    Serikali ya Tanzania imetangaza bajeti yake na kusema inapanga kutumia shilingi za Tanzania trilioni 34.88. Waziri wa fedha wa Tanzania Philip Mpango amesema shilingi trilioni 22.1 kati ya hizo zitatengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na nyingine ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

    Waziri wa fedha wa Uganda Bw. Matia Kasaija amesema ongezeko la uchumi wa Uganda limepungua hadi asilimia 3.1 katika mwaka wa fedha wa 2019/20 kutokana na janga la COVID-19. Amesema bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/21 itaunga mkono ufufukaji wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako