• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump ataka kuwawekea vikwazo maofisa wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC

    (GMT+08:00) 2020-06-12 09:24:43

    Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa Marekani itawawekea vikwazo vya kiuchumi na kuwazuia kuingia nchini humo maofisa wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC walioshiriki kwenye uchunguzi kuhusu vitendo vya Marekani katika vita dhidi ya Afghanistan.

    Bw. Trump amesema Marekani si nchi mwanachama wa ICC, kwa hivyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwasimamia wamarekani. Amesema uchunguzi unaofanywa na ICC dhidi ya maofisa wa kijeshi na ujasusi wa Marekani nchini Afghanistan unatishia mamlaka, usalama wa taifa na sera za diplomasia za Marekani.

    Vyombo vya habari vya Marekani vimesema Afghanistan ni nchi mwanachama wa ICC, hivyo mahakama hiyo ina mamlaka ya kuchunguza uhalifu uliotokea nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako