• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Sudan wasifu uungaji mkono wa timu ya matibabu ya China kwenye mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-12 09:35:47

    Maofisa na wataalamu wa Sudan wamesifu ziara ya timu ya matibabu ya China nchini Sudan, ambayo Alhamisi ilikamilisha majukumu ya wiki mbili ya kuisaidia Sudan kupambana na COVID-19.

    Mkurugenzi wa Idara kuu ya Tiba ya Wizara ya Afya ya Sudan Bi. Nada Bakri, amesema wataalamu wa China wana uzoefu mkubwa wa kupambana na COVID-19, ikiwa ni pamoja na kugundua na kutibu ugonjwa huo, na kufanya maamuzi yanayohusiana na kuzuia na kuikinga jamii dhidi ya janga hilo.

    Pia amesema wataalamu wa matibabu wa China walikutana na wenzao wa Sudan walioteuliwa kuweka itifaki na mipango kuhusu kinga na tiba ya COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako