• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini kuimarisha nguvu ya kijeshi ili kukabiliana na tishio la muda mrefu la Marekani

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:25:43

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Bw. Ri Son Gwon amesema, nchi hiyo haijapendezwa na sera ya Marekani kwa Korea Kaskazini, na itazidi kuimarisha nguvu ya kijeshi ili kukabiliana na tishio la muda mrefu la Marekani na kuichukulia kama lengo la kimkakati lisilobadilika.

    Bw. Ri amesema, tangu mazungumzo kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani yafanyike miaka miwili iliyopita, ili kujenga tena uaminifu kati ya nchi hizo mbili, viongozi wa nchi hiyo wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga eneo la majaribio la silaha za nyuklia lililoko kaskazini mwa nchi hiyo, kuirudishia miili ya wanajeshi wa Marekani na kuwaachia wahalifu wa Marekani. Lakini Marekani imekubali kwa maneno kuboresha uhusiano na Korea Kaskazini, lakini kivitendo Marekani inaendelea kuhatarisha hali ya peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako