• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China amtumia salamu za pole rais mteule wa Burundi kutokana na kifo cha rais Nkurunziza

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:28:52

    Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pole rais mteule wa Burundi Evariste Ndayishimiye kutokana na kifo cha rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo.

    Rais Xi, kwa niaba ya serikali na watu wa China, ametoa salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa za rais Nkurunziza na wananchi wa Burundi.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, rais Nkurunziza alikuwa ni mwanasiasa mashuhuri wa Burundi, ambaye aliwaongoza wananchi wake kulinda mamlaka ya nchi, kupinga uingiliaji wa nje wa mambo ya ndani, kuhimiza amani, na utulivu na maendeleo ya nchi hiyo. Amesema China inapenda kuendelea kushirikiana na Burundi, kuhimiza ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo kwa kina, ili kuwanufaisha zaidi nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako