• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisi ya Kamishna wa Wizara ya Mambo ya Nje katika mkoa wa Hong Kong yapinga Uingereza kuingilia kati masuala ya Hong Kong

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:34:30

    Ofisi ya Kamishna wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong imelaani vikali na kupinga Uingereza kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong na China.

    Ofisi hiyo imesema, kwa kutoa mara kwa mara kinachoitwa Ripoti ya kila Miezi Sita kuhusu Hong Kong, Uingereza imeingilia wazi masuala ya Hong Kong na mambo ya ndani ya China, kukiuka kanuni ya sheria ya kimataifa na msingi unaosimamia uhusiano wa kimataifa.

    Kutokana na Uingereza kutumia Azimio la China na Uingereza kuhalalisha kuingilia kati masuala hayo, Ofisi hiyo imesema waraka huo unahusiana na Hong Kong kurejea China na mipangilio husika wakati wa kipindi cha mpito, na haukuipa Uingereza wajibu wowote juu ya Hong Kong baada ya eneo hilo kurejea kwenye China bara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako