• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka jamii ya kimataifa kuendelea kuisaidia Mali

    (GMT+08:00) 2020-06-12 19:39:15

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema Mali inajitahidi kutimiza utulivu wa kisiasa, lakini bado inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ugaidi na janga la COVID-19, na jamii ya kimataifa inapaswa kuendelea kutoa msaada kwa nchi hiyo.

    Bw. Guterres amesema hayo katika mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Mali uliofanyika kwa njia ya video. Ameongeza kuwa kuijenga Mali kuwa na utulivu wa kisiasa na usalama kunahitaji ahadi ya pamoja na endelevu na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINU) kuendelea kuiunga mkono.

    Aidha Bw. Guterres amepongeza juhudi za serikali ya Mali katika kukabiliana na msukosuko huo na kuwataka viongozi wa Mali kuchukua hatua kali zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako