• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Uhuru Kenyatta asema hatua kali, juhudi za pamoja zimesaidia kupunguza kuenea kwa kasi kwa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-13 18:52:14

    Rais Uhuru Kenyatta wa amesema hatua za haraka na ushirikiano miongoni mwa nchi za Afrika vimesaidia kupunguza kuenea kwa virusi vya Corona barani Afrika.

    Rais Kenyatta amesema hayo kwenye mkutano ulioitishwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, na kushikirisha wakuu wa jumuiya za kikanda za uchumi za Umoja wa Afrika.

    Rais Kenyatta pia amezitaka nchi za Afrika kuiga uwezo wa ubunifu ulioonyeshwa na vijana wa bara la Afrika wakati wakitoa mikakati ya kupunguza madhara ya virusi vya Corona.

    Akiongea kwa niaba ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kwa sasa eneo lake linakabiliwa na changamoto ya kuoanisha itifaki ya mwitikio wa kupambana na virusi vya Corona, lakini amewahakikishia kuwa uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wataendelea kufanya kazi pamoja kuhakikisha mizigo inasafirishwa kati ya nchi wanachama, huku watu wakilindwa dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako