• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maambukizi ya virusi vya Corona yaendelea kwa kasi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-13 18:58:24

    Ofisi ya Shirika la Afya Duniani WHO barani Afrika tarehe 11 mwezi Juni ilitoa habari kuwa, tangu kuripotiwa kwa mtu wa kwanza aliyeambukizwa virusi vya Corona barani Afrika katikati ya mwezi Februari, hivi sasa idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo imezidi laki 2, na watu zaidi 5,600 wamekufa kutokana na virusi vya Corona, na maambukizi ya virusi hivyo bado yanazidi kuenea.

    Takwimu kutoka idara hiyo zinaonesha kuwa miongoni mwa nchi 54 za Afrika, maambukizi katika nchi 10 yanachukua asilimia 80 ya jumla. Afrika Kusini imeathiriwa zaidi, na inachukua asilimia 25 ya kesi za maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako