• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa polisi ya Atlanta ajiuzulu baada ya afisa wa polisi kumpiga risasi na kumuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-14 19:09:18

    Mkuu wa polisi ya Atlanta Erika Shields amejiuzulu jana Jumamosi baada ya afisa Garrett Rolfe kumpiga risasi na kumuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika Rayshard Brooks, Ijumaa usiku katika jimbo la Georgia.

    Kwenye mkutano na wanahabari, meya wa mji wa Atlanta Keisha Lance ametangaza uamuzi wa Shields huku akitoa wito wa kufukuzwa kazi mara moja afisa huyo aliyemuua Brooks. Rayshard mwenye miaka 27 alipigwa risasi na kuuawa baada ya polisi kupokea malalamiko kwamba alikuwa amelala kwenye gari katika barabara ya mgahawa wa Wendy. Polisi wamesema walijaribu kumshikilia Brooks baada ya kupimwa na kupatikana amelewa, na ndipo hapo ikapelekea msokotano kati ya polisi na Brooks ambapo hatimaye alipigwa risasi na baadaye kufa hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji.

    Tukio hili limetokea siku chache tu baada ya kifo cha George Floyd Mmarekani mwenye asili ya Afrika, akiwa mikononi mwa polisi na kuchochea maandamano makubwa katika nchi nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako