• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mteule wa Burundi kuapishwa kuwa rais kufuatia kifo cha Nkurunziza

    (GMT+08:00) 2020-06-15 09:01:31

    Mahakama ya kikatiba nchini Burundi Ijumaa iliyopita ilitangaza kuapishwa kwa rais mteule Evariste Ndayishimiye "haraka iwezekanavyo", kufuatia kifo cha rais Pierre Nkurunziza.

    Bw. Ndayishimiye, aliyepata ushindi kwenye uchaguzi wa Mei 20, alikuwa anatarajiwa kuchukua madaraka kutoka kwa rais Nkurunziza mwezi Agosti wakati muda wake utakapomalizika. Lakini kifo cha ghafla cha rais Nkurunziza kutokana na mshutuko wa moyo Jumatatu iliyopita kiliweka uwekezano kwa spika wa Bunge la Burundi Bw. Pascal Nyabenda kuwa kaimu rais, kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Ndayishimiye kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako