• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamisheni ya afya ya China yaitaka Beijing kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-15 09:53:55

    Kamisheni ya Afya ya Taifa ya China imeuongoza mji wa Beijing kufanya kazi ya kinga na udhibiti wa virusi vya Corona, na kuutaka mji wa Beijing kuchukua hatua madhubuti za kinga na tiba, ili kuzuia maambukizi kabla ya kuenea zaidi.

    Kamisheni hiyo imeutaka mji wa Beijing kupanua kazi ya kuchukua sampuli za mazingira na vitu katika masoko ya bidhaa za kilimo mjini Beijing, kupanua vipimo kwa maeneo na watu wanaotiliwa shaka, kupanua uchunguzi kwa watu waliokaribiana na wagonjwa, na kupanua idadi ya watu wanaowekwa karantini. Kuimarisha usimamizi na uchunguzi wa kimatibatu, kuimarisha udhibiti wa maambukizi ya hospitali, kuimarisha kuripoti na kutangaza habari za maambukizi na kuimarisha elimu kwa umma.

    Kamati hiyo pia inataka kugundua mapema, kuripoti mapema, kutengwa mapema na kutibu mapema wagonjwa wa virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako