• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin wa Russia asema hali ya hivi karibuni nchini Marekani imeonesha msukosuko wa ndani nchini humo

    (GMT+08:00) 2020-06-15 10:15:41

    Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa maoni yake kuhusu hali ya hivi sasa nchini Marekani katika Kipindi cha maongezi kinachoitwa "Moscow·Kremlin·Putin", akisema hali ya hivi karibuni ya Marekani imeonesha msukosuko wa kina wa ndani nchini humo.

    Habari kutoka Shirika la Habari la Itar-Tass la Russia limesema, mwanamume mwenye asili ya Afrika George Floyd aliuawa baada ya kukandamizwa shingoni na polisi mzungu mjini Minneapolis, tukio ambalo limesababisha maandamano makubwa ya kupinga mauaji yake katika sehemu mbalimbali nchini humo.

    Rais Putin akizungumzia tukio hilo amesema, tatizo la mfumo wa kisiasa wa Marekani ni kuwa unatoa kipaumbele maslahi ya vyama kuliko ya wananchi. Amesisitiza kuwa Baraza la Mawaziri la Russia na maofisa waandamizi katika sehemu mbalimbali wanaweza kufanya kazi kwa ushirikiano, na kuweza kushinda maambukizi ya virusi vya Corona kwa kupata hasara ndogo, lakini Marekani haiwezi. Pia ameeleza kuwa suala la ubaguzi wa rangi nchini Marekani linaweza kuleta janga la kuangamiza, na kwamba Russia inapaswa kudumisha masikilizano kati ya makabila mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako