• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wenye asili ya Afrika watoa wito wa kumaliza ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2020-06-15 17:12:40

    Zaidi ya maofisa 20 wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wenye asili ya Afrika ama Waafrika wameeleza hasira yao juu ya kuenea kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi.

    Maofisa hao ambao waliorodhesha majina yao kwenye taarifa yao ya pamoja, ni pamoja na wakuu wa mashirika ya Umoja huo akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dr. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mtendaji wa Programu ya Pamoja ya UKIMWI ya Umoja huo Bi. Winnie Byanyima, na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa, Bi. Natalia Kanem.

    Taarifa ya viongozi hao imezungumzia kifo cha George Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika ambaye alifariki baada ya polisi kumkandamiza kwa goti shingoni kwa zaidi ya dakika nane. Taarifa hiyo imesema sasa ni wakati wa kuendelea mbele zaidi ya kulaani vitendo vya kibaguzi, ambavyo ni tatizo la dunia lililoendelezwa kwa miongo kadhaa.

    Viongozi hao pia wameutaka Umoja wa Mataifa kusimama na kuchukua hatua za uhakika ili kusaidia kumaliza mfumo wa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika na makundi mengine madogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako