• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema njama ya Marekani kuhusika katika kukamatwa kwa Meng Wanzhou imefichuliwa

    (GMT+08:00) 2020-06-15 18:03:10

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, imebainika tena kuwa kukamatwa kwa ofisa mkuu wa fedha wa kampuni ye teknolojia ya China Huawei Bibi Meng Wanzhou ni njama ya kisiasa.

    Ijumaa iliyopita, Mahakama ya Canada iliweka wazi kumbukumbu moja iliyotolewa tarehe mosi, Disemba mwaka 2018 na shirika la ujasusi la Canada kuwa Shirika la Upelelezi la Marekani FBI lililiarifu shirika hilo kuhusu mpango wa kukamatwa kwa Bibi Meng muda mfupi kabla ya kukamatwa kwake katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vancouver. Kumbukumbu hiyo ilisema FBI haikushiriki kwenye operesheni hiyo ili kuepusha watu kuona kuwa Marekani ilitoa shinikizo kwa Canada.

    Akizungumzia hilo, Zhao amesema kumbukumbu hii imefichua njama ya kisiasa ya Marekani ya kukandamiza kampuni za teknolojia ya juu za China ikiwemo Huawei, na Canada ni mshirika wa Marekani.

    Amesisitiza kuwa China ina nia thabiti ya kuwalinda raia wake na maslahi halali za kampuni za China, na kuitaka Canada iangalie kwa makini msimamo imara na ufuatiliaji wa China, kumwachia huru mara moja Bibi Meng, na kumruhusu arudi China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako