• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wa Marekani afungwa miaka 16 nchini Russia kwa kosa la kufanya ujasusi

    (GMT+08:00) 2020-06-15 19:18:50

    Mahakama ya Mjini Moscow, imemhukumu raia wa Marekani Paul Whelan kifungo cha miaka 16 jela baada ya kumkuta na hatia ya kufanya ujasusi nchini Russia.

    Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kumhukumu Whelam, askari wa zamani wa jeshi la majini la Marekani, kifungo cha miaka 18 jela.

    Katika mahakama hiyo, Whelan alieleza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, akidai kuwa hakutenda kosa hilo.

    Wakili wake Bw. Vladmir Zherebenkov amewaambia wanahabari kuwa, baada ya kukata rufaa wataamua kama wataomba msamaha ama kubadilishana wafungwa raia wa Russia Konstatin Yaroshenko au Viktor Bout waliofungwa nchini Marekani.

    Whelan alikamatwa Disemba 28, 2018 mjini Moscow na Idara ya Usalama ya Russia kwa kushukiwa kuwa jasusi, ingawa familia yake ilisema alikwenda Moscow kuhudhuria harusi ya rafiki yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako