• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Korea Kusini atarajia njia ya mazungumzo itasaidia kufikia mwafaka na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2020-06-15 20:07:22

    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini leo kwenye ikulu yake amesema anatrajia kuwa nchi hiyo na Korea Kaskazini zinaweza kufikia mwafaka kwa njia ya majadiliano.

    Rais Moon amesema, anafahamu nia na juhudi za Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un kuhusu kubadilisha mazingira ya peninsula ya Korea kwa njia ya kihistoria, lakini pia kusikitishwa na kukosekana kwa maendeleo ya uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini, na uhusiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini kama inavyotarajiwa.

    Amesema umefika wakati kwa Korea Kusini na Korea Kaskazini kushirikiana kutafuta njia ya kupata mafanikio kwa pamoja, na pia wakati umefika ambapo nchi hizo mbili hazitakaa na kusubiri mazingira yaboreshwe. Amesema anatarajia Korea Kaskazini itafungua milango yake kwa ajili ya majadiliano na kubadilishana maoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako