• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muda wa mpito wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya kwisha Desemba 31 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:11:00

    Viongozi wa Umoja wa Ulaya na waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson jana walifanya mkutano kwa njia ya video, ambapo pande hizo mbili zimethibitisha kuwa muda wa mpito wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya hautarefushwa na utakwisha tarehe 31 Desemba mwaka huu, bila kujali matokeo ya mazungumzo kuhusu uhusiano kati yao katika siku za baadaye.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Ulaya imesema mazungumzo ya hivi sasa kuhusu uhusiano kati ya umoja huo na Uingereza katika siku za baadaye yanahitaji "kasi mpya", hivyo pande hizo mbili zitaharakisha mchakato wa mazungumzo mwezi Julai, ili kujaribu kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kukamilisha na kupitisha makubaliano kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako