• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafahamisha uzoefu wa kupambana na COVID-19 kwa kutumia teknolojia ya nyukilia

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:11:29

    Mkutano wa Bodi ya Magavana ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA umefanyika jana kwa njia ya video, ambapo mkurugenzi wa shirika la nishati ya atomiki la taifa la China Bw. Zhang Kejian, ameeleza uzoefu wa China katika kupambana na COVID-19 kwa kutumia teknolojia ya nyukilia.

    Bw. Zhang amesema China imetumia mionzi ya nyuklia katika kuua vijidudu kwenye vifaa tiba, na kuinua kidhahiri kiwango cha ufanisi wa kazi hiyo. Kwenye maeneo yaliyokumbwa na janga la COVID-19, teknolojia ya mionzi ya nyukilia ilitumika katika kushughulikia maji taka ya matibabu na kupata mafanikio makubwa.

    Hivi karibuni mradi mkubwa zaidi wa kushughulikia maji taka ya viwanda kwa kutumia teknolojia ya mionzi ulizinduliwa nchini China, hii imeonesha kuwa teknolojia ya China ya kushughulikia uchafuzi kwa nyukilia imeanza kutumika kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako