Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Misri Bw. Ahmad Hafez amesema Misri itaomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuizuia Ethiopia kuchukua hatua yoyote kuhusu bwawa kubwa la Ethiopia GERD.
Bw. Ahmad amesema hatua yoyote ya upande mmoja ya Ethiopia itaathiri vibaya haki ya Misri katika mto wa Nile na amani na usalama wa kimataifa.
Bw. Ahmad ameongeza kuwa katika miaka michache iliyopita, Misri imejaribu kufikia makubaliano ya kusuluhisha mgogoro wa GERD pamoja na kulinda maslahi ya Ethiopia na Sudan, lakini mazungumzo ya hivi karibuni hayajaleta matokeo yoyote mazuri. Misri, Ethiopia, na Sudan zimeamua kuendelea na mazungumzo kwa njia ya video Jumatatu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |