• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki na Russia zaendelea kushirikiana ili kutimiza usitishaji vita wa kudumu nchini Libya

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:17:26

    Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Bw. Mouloud Gawish Oglu amesema Uturuki itaendelea kushirikiana na Russia ili kutimiza usitishaji vita wa kudumu nchini Libya.

    Bw. Gawish Oglu amefanya mazungumzo na mwenzake wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif huko Istanbul na kusema Uturuki na Russia hazina tofauti yoyote juu ya kanuni za kimsingi kuhusu suala la Libya, na pande hizo mbili zitafanya mazungumzo ya mawaziri wakati masuala yote yakiwa wazi.

    Kwa upande wake Bw. Zarif amesema wamejadili suala la kufungua tena mpaka kati ya nchi hizo mbili na kurejesha safari za ndege za kimataifa kati ya nchi hizo mbili, pia wamefanya mazungumzo ya kiujenzi, na kubadilishana maoni kuhusu ushirikiano wa pande mbili, masuala ya kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako