• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasaidia shule ya Zambia katika kupambana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:40:27

    Ofisa wa serikali ya Zambia amesema Shirikisho la Zambia-China limechangia vifaa tiba kwa shule ya msingi ya Evergreen iliyoko eneo la Chongwe mkoani Lusaka nchini humo.

    Kamishna wa eneo la Chongwe Bw. Robster Mwanza amesema vifaa hivyo vyenye thamani ya takriban dola elfu mbili za kimarekani ikiwa ni pamoja na barakoa, glavu, vitakasa mikono, na taulo za kike, vitu ambavyo vitasaidia shule iliyoko kijiji cha Kanakantapa katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona. Ameongeza kuwa taulo za kike zitaongeza mahudhurio ya wasichana shuleni, ambao wanakumbwa na changamoto ya kununua vitu hivyo kutokana na janga la virusi vya Corona.

    Amelishukuru shirikisho hilo kwa kuiunga mkono shule hiyo, ambayo itanufaika na vifaa hivyo kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako