• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yapanga kuwapatia mafuta wafanyakazi walioko mstari wa mbele wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-16 09:40:49

    Waziri wa nishati na umeme wa Zimbabwe Bw. Fortune Chasi amesema serikali ya Zimbabwe inapanga kuweka vituo maalumu vya mafuta ya petroli kwa ajili ya wafanyakazi walioko mstari wa mbele wa kupambana na virusi vya Corona.

    Amesema kazi za madaktari, wauguzi, polisi na wafanyakazi wa ulinzi zimesumbuliwa kutokana na upungufu wa mafuta nchini humo, hali ambayo inawabidi watu hao wasubiri kwa muda mrefu foleni kupata mafuta. Serikali inatunga mkakati wa kujenga vituo hivyo maalumu vya mafuta, ili kuwasaidia wafanyakazi hao waweze kumaliza kazi zao kwa wakati.

    Kwa sasa, Zimbabwe inapambana na msukosuko wa kiuchumi ambao ni mkubwa zaidi kutokea ndani ya miaka 10 iliyopita kutokana na ukosefu mkubwa wa fedha za kigeni zinazohitajika kuagiza bidhaa za kimsingi kutoka nje ikiwemo mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako