• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • George Muntu: kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona kwa mshikamano na ushirikiano

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:40:49

    Tarehe 13 Juni, gazeti la Daily News la Tanzania lilichapisha makala ya George Muntu yenye kichwa cha "Kupambana na maambukizi ya COVID-19 kwa mshikamano na ushirikiano". Makala hiyo inaeleza maudhui na umuhimu wa hotuba ya rais Xi Jinping wa China katika ufunguzi wa mkutano wa 73 wa afya duniani.

    Anaona China siyo tu imedhibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchini China, bali pia inatoa msaada kwa nchi nyingine hasa nchi zinazoendelea kupambana na virusi hiyo, na kuonyesha majukumu yake ya kuwa nchi kubwa. Yaliyomo kwenye makala hiyo yanasema:

    Kwenye ufunguzi wa mkutano wa 73 wa afya duniani uliofanyika Tarehe 18 Mei, rais Xi Jinping wa China alitoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na kushirikiana katika kupambana na virusi vya Corona. Hotuba hiyo inalenga kuinua imani ya dunia ya kupambana na virusi hiyo, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na kuboresha mfumo wa usimamizi wa afya duniani katika siku za mbele.

    Tangu maambukizi ya virusi vya Corona yalipoibuka, China siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na virusi hiyo na kuzisaidia nchi nyingine kupambana na msukosuko huo mbaya zaidi wa afya ya umma duniani. Tofauti na nchi zilizoendelea, China siyo tu inashughulikia kulinda afya na usalama wa watu wake, pia inasaidia nchi nyingine hasa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo kujenga mfumo wa afya ya umma.

    Hadi kufikia tarehe 31 Mei, China imetoa msaada wa vifaa tiba vya kupambana na virusi vya Corona kwa nchi 150 na mashirika 4 ya kimataifa, kutuma timu 29 za wataalamu wa matibabu kwa nchi 27. China pia imefanya shughuli zaidi 70 za mawasiliano kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona na mashirika ya kimataifa na ya kikanda na nchi husika zikiwemo Umoja wa Afrika.

    Tunatakiwa kukumbuka kuwa wakati Italia na Hispania zilipokumbwa na mlipuko wa virusi hiyo, ni China na sio nchi nyingine za Umoja wa Ulaya au NATO zilizotoa msaada, kuchangia vifaa tiba vinavyohitajika, na kutuma wataalamu wa matibabu.

    Mshikamano na ushirikiano ni silaha yenye nguvu ya kupambana na virusi, kukabiliana na msukosuko wa afya ya umma duniani, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kuondoa tofauti za mashariki na magharibi, kusini na kaskazini, kujenga kwa pamoja jumuiya yenye hatma ya pamoja ya afya ya binadamu. China si kama tu inasema hiyo, bali pia inatekeleza hivyo. China kwa mara nyingine tena imeonyesha kwa dunia nzima majukumu yake ya kuwa nchi kubwa. Sisi waafrika tunapaswa kutambua kuwa, China iko pamoja na Afrika, na siku zote itaendelea kuwa bega kwa bega na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako