• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasheria wa Meng Wanzhou waona Benki ya HSBC ilishirikiana na Marekani kumsingizia Meng Wanzhou

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:46:13

    Tarehe 15 Jun, kesi ya kumkabidhi Bibi Meng Wanzhou kwa upande wa Marekani ilisikilizwa tena huko Vancouver, Canada. Timu ya wanasheria wa Meng Wanzhou iliwasilisha kumbukumbu kwenye Mahakama Kuu ya British Columbia ya Canada, ikionesha kuwa ushahidi muhimu uliowasilishwa na Wizara ya sheria ya Marekani ya kutaka kukabidhiwa kwa Meng Wanzhou ulitolewa na Benki ya HSBC, lakini ushahidi huo unakosa taarifa muhimu, na hata unapotosha ukweli kwa makusudi.

    Kumbukumbu hiyo imeonesha kuwa mwezi Desemba mwaka 2012, Benki ya HSBC iliipa Wizara ya Sheria ya Marekani faini ya dola za kimarekani bilioni 1.9 kutokana na ukiukaji wake yenyewe, na kusaini Mkataba wa kusimamisha mashtaka na Marekani. Tarehe 22 Agosti mwaka 2013, Bibi Meng Wanzhou alitoa hotuba ya PPT kwa ofisa mwandamizi wa benki ya HSBC huko Hongkong, PPT hiyo iliwasilishwa na HSBC kwa Marekani, ikiwa ushahidi kwa mahakama ya Canada ya kuamini kuwa Meng Wanzhou aliidanganya Benki ya HSBC.

    Lakini kumbukumbu ya kesi hiyo ya Marekani imekiri kuwa, mfanyakazi wa kawaida wa Benki ya HSBC anajua uhusiano kati ya Kampuni ya Huawei na kampuni ya Skycom, huku ikidai kuwa wasimamizi waandamizi wa benki hiyo hawajui hali hii. Wanasheria wa Meng Wanzhou wanaona kauli hii haiaminiki, na watatoa ushahidi zaidi kuthibitisha kuwa ni "uwongo mkubwa".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako