• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya wataalamu wa afya ya China iliyotumwa Algeria na Sudan yarudi nchini baada ya kukamilisha majukumu

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:51:40

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, amesema timu ya wataalamu wa matibabu iliyotumwa na serikali ya China nchini Algeria na Sudan imerudi China baada ya kukamilisha majukumu yao.

    Kutokana na mwaliko wa serikali za Algeria na Sudan, timu hiyo yenye wataalamu 20 Mei 14 iliwasili nchini Algeria na kuanza operesheni ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Bw. Zhao amesema wakati timu hiyo ikifanya kazi nchini Algeria na Sudan, wataalamu walibadilishana uzoefu na maofisa wa serikali za nchi hizo mbili, wataalamu, wajumbe wa shirika la afya duniani na madaktari wa hospitali za huko kupitia mazungumzo, utoaji wa mafunzo, uchunguzi na mijadala kuhusu COVID-19, huku wakijadili hatua za kinga na tiba ya ugonjwa huo na kutoa mapendekezo. Wataalamu hao pia wametembelea hospitali, maabara, taasisi za nchi hizo mbili na kutoa mafunzo maalumu kwa madaktari wa nchi hizo mbili ambayo yalihudhuriwa na watu zaidi ya 5,400.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako