• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping kuendesha mkutano wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-16 10:56:00

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo ametangaza kuwa, rais Xi Jinping wa China kesho hapa Beijing ataendesha na kuhutubia mkutano maalumu wa kilele wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Mkutano huo umefanyika chini ya pendekezo la pamoja la China, nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika Afrika Kusini, na nchi mwenyekiti wa pamoja wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika Senegal, ambapo viongozi wa nchi wanachama wa baraza la mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, nchi wenyekiti wa zamu wa jumuiya za kikanda za Afrika, na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika watashiriki. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkurugenzi mkuu wa WHO pia wamealikwa kuhudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako