• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yasema Korea Kaskazini imevunja ofisi ya uhusiano iliyopo Kaesong

    (GMT+08:00) 2020-06-16 17:21:27

    Wizara ya Muungano ya Korea Kusini imesema, Korea Kaskazini jana imelipua kwa bomu ofisi ya uhusiano iliyoko kwenye mji wa mpaka wa Kaesong.

    Vyombo vya habari nchini humo vimenukuu chanzo cha kijeshi kikisema, mlipuko ulisikika na moshi kuonekana katika Bustani ya Viwanda ya Kaesong, ambalo ni eneo la viwanda linalojumuisha nchi hizo mbili, na ambako pia ni sehemu ilipo ofisi hiyo ya uhusiano.

    Ofisi hiyo ilifunguliwa Septemba mwaka 2018 kwa ajili ya mawasiliano ya saa 24 kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini, kama ilivyoelekezwa katika Azimio la Panmunjom. Azimio hili lilisainiwa na waziri wa Korea Kusini Moon Jae-in na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un baada ya mkutano wao wa kwanza uliofanyika April, 2018 katika kijiji cha upatanishi cha Panmunjom.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako