• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya mjadala wa dharura kuhusu ubaguzi

    (GMT+08:00) 2020-06-16 18:33:07

    Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeamua kufanya mjadala wa dharura kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu unaotokana na ubaguzi unaotokea sasa mara litakapoanza mkutano wake wa 43 jumatano wiki hii.

    Katika taarifa yake, Baraza hilo limesema mjadala huo utalenga ukiukaji wa haki za binadamu unaotokana na ubaguzi wa rangi, mfumo wa kibaguzi, ukatili unaofanywa na polisi, na ukatili wanaofanyiwa watu wanaoandamana kwa amani.

    Mjadala huo unafanyika kutokana na ombi lililotolewa na Burkina Faso kwa niaba ya Kundi la Afrika, ambalo ni kundi la kikanda la Umoja wa Mataifa linalojumuisha nchi za Afrika.

    Katika barua yake kwa Baraza hilo, Burkina Faso imesema kifo cha George Floyd katika mji wa Minneapolis nchini Marekani sio tukio la kipekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako