• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Usafirishaji Baharini ya China yatoa msaada wa magari Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2020-06-16 18:38:22

    Kampuni ya Usafirishaji wa Mizigo Baharini ya Maersk na Kampuni ya Usafiri wa Majini ya China zimesaini makubaliano ya kupanua mtandao wao katika kanda ya Afrika Mashariki.

    Katika huduma hiyo ya pamoja iliyopewa jina la "Mashariki", kampuni hizo mbili kubwa zitahakikisha huduma bora kwa bandari za Mombasa nchini Kenya na Dar es Salaam nchini Tanzania.

    Makubaliano hayo yaliyosainiwa Mei 21 yanalenga kuboresha bandari ya Mombasa kwa kuwa itaunganika moja kwa moja na bandari ya Shanghai nchini China. Hatua hiyo itawapatia wateja wanaotumia bandari ya Mombasa fursa kubwa ya kufikia moja ya masoko makubwa nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako