• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuendesha mkutano wa ngazi ya juu wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja na Njia Moja

    (GMT+08:00) 2020-06-16 18:49:56

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian leo amesema, waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ataongoza mkutano wa ngazi ya juu wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja utakaofanyika Alhamis wiki hii kwa njia ya video.

    Amesema mkutano huo utajadili mada ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na ushirikiano katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona. Mkutano huo utawakutanisha mawaziri na maofisa wa ngazi ya mawaziri wa nchi 25, na wakuu wa Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani.

    Mkutano huo unalenga kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika baraza la pili la viongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Ukanda Mmoja , Njia Moja, kuhimiza nchi zilizojiunga na pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kwa kupambana na virusi vya Corona, na kuanzisha mawasiliano ya uzoefu wa kuanza tena uzalishaji na utengenezaji, na kujenga pendekezo hilo kwa kiwango kikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako