• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano maalum wa ushirikiano wa kupambana na virusi vya Corona kati ya China na Afrika kufanyika kesho

    (GMT+08:00) 2020-06-16 19:31:00

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, Rais Xi Jinping wa China ataongoza mkutano maalum wa ushirikiano wa kupambana na virusi vya Corona kati ya China na Afrika utakaofanyika kesho kwa njia ya video.

    Bw. Zhao amesema, China inaendelea kuzingatia kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na Afrika, na kujitahidi kushirikiana na nchi za Afrika kujenga jumuiya nzuri zaidi yenye hatma ya pamoja kati yao. Tangu kutokea kwa mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona, China na Afrika zimesaidiana na kupambana kwa pamoja na virusi hivyo na kuufanyia uhusiano kati yao ufikie ngazi ya juu zaidi.

    Habari zinasema, mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe kutoka Umoja wa Afrika na mashika mengine muhimu ya Afrika, pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako