• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yathibitisha kesi 106 za maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya siku 5

    (GMT+08:00) 2020-06-16 19:31:25

    Naibu mkuu wa idara ya uenezi katika manispaa ya Beijing, Bw. Xu Hejian amesema, tangu tarehe 11, mwezi huu, Beijing imeripoti kesi 106 za maambukizi ya virusi vya Corona, na kufanya kazi za kukinga maambukizi ya virusi hivyo uwe muhimu zaidi.

    Bw. Xu amesema, hivi sasa, ni lazima wakazi wa mji huo wachukue hatua kali kwa haraka, kutafuta watu wote waliotembelea soko la Xinfadi na kuwafanyia vipimo vya virusi vya Corona, na kuwaweka karantini ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa masoko mjini Beijing Bw. Chen Yankai amesema, idara hiyo imepuliza dawa za kuwaua vijidudu na virusi katika masoko 276 ya kilimo na kuongeza usimamizi katika masoko na kudhibiti vitendo vya kuongeza ovyo bei za chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako