• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 24 wa Mali wauawa katikati ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2020-06-16 19:46:47

    Jeshi la Mali jana usiku limethibitisha kuwa askari 24 wameuawa katika shambulizi lilitokea jumapili huko Diabaly, mkoa wa kati wa Segou.

    Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya jeshi hilo imesema, askari wanane wameokolewa, na uchunguzi juu ya hali hiyo unaendelea na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

    Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limekiri kuwajibika na shambulio hilo. Lakini wachunguzi walisema kuwa shambulio hilo labda lilifanywa na kundi la ugaidi katika mkoa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako