• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ICRC yaeleza wasiwasi juu ya maambukizi ya COVID-19 katika kambi za wakimbizi Somalia

    (GMT+08:00) 2020-06-17 09:28:41

    Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC jana jumanne ilieleza wasiwasi kuhusu maambukizi ya COVID-19 yanayoweza kuibuka bila kugunduliwa kwenye kambi zilizojaa wakimbizi nchini Somalia.

    Mratibu wa afya wa ICRC nchini Somalia Bibi Ana Maria Guzman amesema kuweka umbali wa kijamii, kufuata kanuni za usafi na kudumisha afya ni changamoto kubwa inayozikabili kambi hizo, hasa zile za wakimbizi wa ndani.

    Kwa mujibu wa ICRC, mfumo wa huduma za afya wa Somalia umeathiriwa na ukosefu wa uwekezaji na machafuko yaliyodumu kwa miongo kadhaa, na ni asilimia 50 tu ya wakazi wa mijini wanaweza kupata huduma za matibabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako