• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNECA yasema mavumbuzi ya kisayansi na kiteknolojia ni muhimu kwenye ufufuaji wa Afrika wakati wa janga la Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-17 09:52:26

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni katibu mtendaji wa Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA Bibi Vera Songwe, amesema sayansi, teknolojia na uvumbuzi ni muhimu kwenye ufufuaji wa uchumi wa Afrika wakati janga la virusi vya Corona likiendelea.

    Bibi Songwe amesema hayo alipohudhuria Jukwaa la uvumbuzi na uwekezaji la Afrika la mwaka 2020, na kusisitiza kuwa Afrika inahitaji uvumbuzi ili kutatua suala la kudidimia kwa uchumi kutokana na janga la virusi vya Corona. Amesema uwekezaji wa uvumbuzi, sayansi na teknolojia vinahitajika kuwalinda watu wa Afrika na kuondokana na msukosuko huo.

    Ameongeza kuwa teknolojia ni kitu cha kimsingi kwa Afrika katika kuondokana na msukosuko huo kwa njia ya maendeleo endelevu, ambako bara la Afrika linapaswa kujenga miundombinu ya lazima kwa ajili ya kutoa nafasi za ajira zenye ubora, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuhimiza mambo ya afya, na kuwaunga mkono vijana katika kufanya uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako