• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini atoa wito kwa vijana kujenga upya uchumi

    (GMT+08:00) 2020-06-17 09:52:50

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana akihutubia kwenye maadhimisho ya Siku ya Vijana ametoa wito kwa vijana kuwa na mawazo ya uvumbuzi ili kuisaidia serikali kujenga upya uchumi wa nchi.

    Amesmea janga la Corona limewapatia watu mtazamo mpya juu ya kujenga upya uchumi, na vijana wanapaswa kutoa mchango katika kuhimiza mageuzi. Amesema serikali itawapatia vijana fursa za kupata mafunzo ili kuongeza uwezo wao wa kuchochea uchumi.

    Ameongeza kuwa vijana ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi vijijini wanapaswa kupewa fursa ya kupata teknolojia kwa ajili ya masomo na kazi zao, huku biashara zinazoongozwa na vijana zikitakiwa kuongoza kwenye kuleta fursa kwenye jamii zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako