• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapitia upya miongozo ya upimaji wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-17 10:24:45

    Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe ametangaza mpango wa kupitia upya miongozo ya upimaji wa COVID-19 kuendana na magunduzi mapya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu wagonjwa wasio na dalili.

    Bw. Kagwe amesema kwa mujibu wa miongozo ya WHO, wagonjwa wasio na dalili wanapaswa kuwekewa karantini kwa siku tisa hadi kumi, tofauti na wiki mbili inavyotekelezwa nchini humo.

    Bw. Kagwe ameongeza kuwa wagonjwa hao watapatiwa maafisa wa afya ya umma au wafanyakazi wa afya ya jamii kwa ajili ya ufuatiliaji wa kila siku.

    Hadi sasa watu 1,326 wamethibitika kuambukizwa virusi vya COVID-19 nchini Kenya na wagonjwa 105 kati yao wamefariki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako