• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yatangaza mpango wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2021

    (GMT+08:00) 2020-06-17 10:25:26

    Tume ya uchaguzi ya Uganda imetangaza mpango wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2021, ikisisitiza hatua za kuzuia COVID-19.

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo Bw. Simon Byabakama, amesema uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani utafanyika kati ya tarehe 10 mwezi Januari na tarehe 8 mwezi Februari.

    Bw. Byabakama amesema mikutano mikubwa ya kampeni haitaruhusiwa ikiwa ni jitihada za kutekeleza umbali wa kijamii ili kuzuia kuenea kwa COVID-19.

    Aidha tume hiyo itatoa fomu za wagombea kwenye tovuti yake ambazo zinaweza kupakuliwa na wagombea kwenye mtandao.

    Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Uganda, hadi sasa Uganda ina watu 724 waliothibitika kuambukizwa COVID-19, wagonjwa 351 wamepona na hakuna mgonjwa aliyekufa kutokana na ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako