• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kwa nini Afrika imepata matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-17 10:29:10

    Hadi kufikia jumanne idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imezidi laki 2.5, na idadi ya vifo imefikia 6,769 ambayo imedumisha kiwango cha chini cha vifo kuliko cha wastani duniani, hali ambayo ni nzuri kuliko ilivyokadiriwa na wataalamu.

    Hadi sasa ingawa idadi ya maambukizi inaongezeka, kutokana na hatua kali za kinga na udhibiti, idadi kubwa ya vijana na ushirikiano na China, juhudi za kupambana na virusi vya Corona zimepata mafanikio makubwa. Kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha Africa CDC kinasema kuwa nchi karibu 43 za Afrika zimefunga mipaka kutokana na kuenea kwa kasi wa virusi vya Corona. Licha ya hayo, zuio la kutoka nje limetekelezwa katika nchi 35.

    Kwa kuzingatia idadi ya watu, Afrika ina idadi kubwa ya vijana ambayo imeyafanya maambukizi ya COVID-19 kuwa na athari ndogo na dalili ndogo kwa watu hao.

    Vyombo vya habari vimewanukuu wataalamu wa Kenya na Uingereza wakisema, idadi kubwa ya ya vijana barani Afrika wana umri wa wastani wa chini ya miaka 20, ikilinganishwa na watu wa Ulaya na Marekani wenye umri wa wastani wa zaidi ya miaka 38, huenda ni chanzo cha kuwa na idadi ndogo ya maambukizi na vifo.

    Msaada kutoka China pia umefanya kazi muhimu katika mapambano dhidi ya maambukizi hayo barani Afrika. Tangu maambukizi ya virusi vya Corona yaibuke, China na Afrika zimesaidiana na kushirikiana katika mapambano hayo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying tarehe 12 Juni alisema, China imetuma shehena kadhaa za vifaa tiba na timu za wataalamu kwenda katika nchi za Afrika, na kufanya semina 400 za mafunzo kwa makumi ya maelfu ya wafanyakazi wa matibabu wa Afrika.

    China na Afrika ni ndugu na wenzi wazuri wanaokabiliana na taabu kwa pamoja. Kama alivyosema mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat, Afrika na China ni marafiki na muhimu zaidi ni ndugu. Hakuna kinachoweza kubadilisha au kuharibu uhusiano na Urafiki kati ya pande hizo mbili, ambao ni imara na hauvunjiki.

    China itaendesha mkutano maalum wa ushirikiano wa kupambana na virusi vya Corona kati ya China na Afrika kwa njia ya video. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, China inaendelea kuzingatia kuendeleza uhusiano na ushirikiano na Afrika, na kujitahidi kushirikiana na nchi za Afrika kujenga jumuiya nzuri zaidi yenye hatma ya pamoja kati yao. Tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Corona, China na Afrika zimesaidiana na kupambana kwa pamoja na virusi hivyo na kuufanyia uhusiano kati yao ufikie ngazi ya juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako