• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wote waliopewa chanjo ya kwanza ya China dhidi ya virusi vya Corona wathibitishwa kupata kingamwili

    (GMT+08:00) 2020-06-17 10:34:34

    Mkutano wa kuthibitisha matokeo ya majaribio ya Chanjo ya kwanza ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya bidhaa za viumbe ya Wuhan ya China umefanyika jana kwa wakati mmoja mjini Beijing na mkoani Henan. Matokeo yameonesha kuwa baada ya kupewa chanjo aina hiyo, hakuna mtu aliyekuwa na dalili mbaya, na wote wamepata kingamwili dhidi ya virusi vya Corona.

    Majaribio hayo yalifanyika kwa siku 66 chini ya uongozi wa Kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha mkoa wa Henan, na kuonesha matokeo kamili ikiwemo data kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo, pamoja na matokeo ya utafiti kuhusu watu wenye umri tofauti ambao walipewa chanjo kwa kiasi tofauti na kwa utaratibu tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako