• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing yathibitisha kwa hatua ya mwanzo chanzo ya maambukizi ya virusi vya Corona kutoka soko la Xinfadi

    (GMT+08:00) 2020-06-17 10:35:55

    Naibu katibu mkuu wa Serikali ya mji wa Beijing Bibi Chen Bei amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana, kuwa kutokana na uchunguzi wa hatua ya mwanzo, maambukizi ya virusi vya Corona yaliyotokea kwenye Soko la jumla la mazao ya kilimo la Xinfadi mjini Beijing yalisababishwa na mawasiliano ya watu au uchafuzi wa vitu. Mitaa na maeneo yenye kiwango cha juu cha hatari yanatakiwa kufungwa na kudhibitiwa, na watu wanaruhusiwa kuingia lakini hawataruhusiwa kutoka, na kupaswa kukaa ndani na kufanyiwa upimaji.

    Hadi kufikia tarehe 15 Juni, watu 106 walithibitishwa kuwa na virusi vya Corona, 10 kati yao walithibitika kuwa na maambukizi lakini hawana dalili. Maambukizi ya virusi yameenea katika maeneo 9 na mitaa 28, pamoja na mikoa ya Hebei, Liaoning na Shandong.

    Ili kukabiliana na hali hiyo, Beijing itachukua hatua thabiti, kwa wakati na kwa makini zaidi kuzuia maambukizi kwa njia ya kisayansi na kwa ufanisi, na kukata kabisa njia za kuenea kwa maambukizi hayo.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako