• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Australia iache mchezo wa kisiasa kuhusu COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-17 19:37:05

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema, China haina haja kueneza habari zisizo za kweli ili kupata heshima, na kutaka baadhi ya wanasiasa wa Australia kuacha mchezo wa kisiasa kuhusu virusi vya Corona (COVID-19).

    Kauli hiyo imekuja baada ya waziri wa mambo ya nje wa Australia Marise Payne kuzilaani China na Russia kwa kutoa taarifa zisizo kweli, na kusema Australia itaendelea kususia "virusi vya habari".

    Zhao amesema, China inakabiliana na virusi vya Corona kwa kufuata wazo la kuzingatia zaidi watu, na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kwa kufuata wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Mafanikio na mchango wa China vimepongezwa na watu wa China na jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako