• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Africa CDC yatoa sababu za juhudi za kupambana na COVID-19 kufanikiwa katika bara la Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-17 19:44:58

    Hatua za haraka na ushirikiano kati ya nchi za Afrika zimesaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona na kukwepa janga kubwa kutokea barani Afrika.

    Hayo yamesema hivi karibuni na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, kauli ambayo imeungwa mkono na Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika (Africa CDC). Kituo hicho kimesema, mpaka kufikia jana, jumla ya kesi zilizothibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona ilizidi 252,000, na idadi ya vifo ni 6,779, idadi ambayo ni ya chini zaidi ya ile ya dunia na ile ya Marekani na Uingereza.

    Kituo hicho kimesema, nchi 43 za Afrika bado zimefunga mipaka yao wakati huu wa mlipuko, na marufuku ya kutembea usiku imewekwa katika nchi 35, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. Sababu nyingine ni kwamba, mazingira ya kijamii yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza na kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

    Pia Kituo hicho kimeonya kuwa, ingawa Afrika imepata mafanikio mazuri katika kudhibiti janga hilo, bado jamii ya kimataifa inatakiwa kushirikiana pamoja ili kuliunga mkono bara hilo, ambalo liko hatarini zaidi kuathiriwa na janga la virusi vya Corona kutokana na masoko na makazi yenye idadi kubwa ya watu, uhaba wa maji salama na miundombinu hafifu ya sekta ya afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako