• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika kuhusu kushirikiana kupambana na ugonjwa wa COVID-19 wafanyika

    (GMT+08:00) 2020-06-17 20:40:01

    Mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika kuhusu Mshikamano dhidi ya virusi vya Corona umefanyika leo hapa Beijing na kuongozwa na rais Xi Jinping wa China.

    Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video, ulipendekezwa kwa pamoja na China, Afrika Kusini ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, na Senegal, ambayo ni mwenyekiti mwenza wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC.

    Viongozi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wanachama wa Umoja wa Afrika, na wenyeviti wa zamu wa mashirika makubwa ya kikanda ya Afrika, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika wamehudhuria mkutano huo.

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani pia walihudhuria mkutano huo kama wageni waalikwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako