• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa WHO wasema dawa dhidi ya malaria zitasitishwa kwenye majaribio ya mshikamano ya kupambana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-18 09:10:20

    Ofisa wa matibabu wa Idara ya Chanjo na Dawa za Kibiolojia ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Ana Maria Restrepo, amesema dawa dhidi ya malaria kwenye majaribio ya mshikamano ya kupambana na COVID-19 zitasitishwa, kwani hazikupunguza idadi ya vifo vya wagonjwa wa COVID-19.

    Wakati huo huo amesisitiza kuwa hii sio sera ya WHO, na wala si pendekezo la sera la WHO.

    Hapo awali kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkurugenzi wa Miradi ya dharura ya afya wa WHO Bw. Michael Ryan, amesema dawa za malaria aina ya hydroxychloroquine na chloroquine zilijumuishwa katika majaribio yanayoendelea katika nchi nyingi. WHO ilipendekeza kutumia dawa hizo kwenye majaribio ya kutibu wagonjwa wa COVID-19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako