• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande za Sudan Kusini zaondoa hali ya kukwama kwenye ugawaji wa majimbo

    (GMT+08:00) 2020-06-18 09:10:49

    Pande mbalimbali zilizosaini makubaliano ya amani ya mwaka 2018 zimekubaliana kuhusu ugawaji wa majimbo 10 nchini humo, na kuvunja hali ya kukwama ya miezi kadhaa katika utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Sudan Kusini imesema, rais Salva Kiir na makamu wa kwanza wa rais Bw. Riek Machar walikutana huko Juba, ambako walijadili mpango mpya wa ugawaji wa majimbo.

    Kutokana na mpango huo chama cha SPLM kinachoongozwa na rais Kiir kitatawala majimbo sita, chama cha SPLM-IO kinachoongozwa na Bw. Machar kitatawala majimbo matatu, na jimbo lingine litatawaliwa na chama cha SSOA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako