• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la haki za binadamu la UM lafanya mjadala wa dharura kuhusu suala la ubaguzi wa rangi

    (GMT+08:00) 2020-06-18 10:03:32

    Mkutano wa 43 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa umefanya mjadala wa dharura kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, ubaguzi wa rangi wa kimfumo, ukatili wa polisi na maandamano ya kiamani.

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bibi Amina Mohammed amemnukuu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterrez akisema, msimamo wa Umoja wa Mataifa katika suala la ubaguzi wa rangi ni wazi, kwamba unakiuka katiba ya Umoja wa Mataifa na umedharau maadili ya kimsingi. Amesema,

    "katika sehemu mbalimbali za dunia, vizazi vya wajukuu wa Afrika wako nyuma kimaendeleo, hali hiyo inasababishwa na vikwazo vya kimaendeleo yasiyo ya haki. Vilevile kutokana na umaskini na ubaguzi wa rangi wa kimfumo, watu wenye asili ya kiafrika wanaathiriwa zaidi katika janga la virusi vya Corona. Baada ya janga hili kumalizika, tunapaswa kuweka hatua zaidi za utekelezaji wa sheria. "

    Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (UNHCHR) Bibi Michelle Bachelet amesema,

    "tukio la Floyd limekuwa ni matokeo ya matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika, watu wa rangi, na watu wa makabila madogomadogo duniani. "

    Amesema kwa sasa hatua za mara moja zinatakiwa kuchukuliwa katika dunia nzima. Siyo tu kufanya mageuzi au kuweka mashirika maalumu mapya na mashirika ya utekelezaji wa sheria, pia tunahitaji kutatua suala la ubaguzi wa rangi. Ubaguzi huo unadhuru taasisi za serikali, kuongeza hali ya kukosekana kwa usawa, na kusababisha matukio mengi ya ukiukaji wa haki za binadamu. Aidha mzunguko wa kutoadhibiwa kwa wahalifu ni lazima utokomezwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako