• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika ni muhimu kwa dunia kushirikiana kupambana na janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-18 10:12:22

    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema Mkutano maalum wa kilele kati ya China na Afrika ni moja ya majukwaa ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, ambalo ni muhimu kwa dunia kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

    Bw. Tedros amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, akisema katika hali ya janga la COVID-19, China, Afrika Kusini na Senegal zimependekeza kwa pamoja kufanyika kwa mkutano huo wenye ajenda maalum ya kupambana na COVID-19.

    Bw. Tedros ameshukuru uungaji mkono wa China kwa Afrika, akisema tangu mlipuko wa janga la COVID-19 ulipoanza, siku zote China inaiunga mkono Afrika, imetuma wataalamu, kubadilishana uzoefu, na kutoa misaada ya vifaa tiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako